Azam FC
imeshindwa kuonyesha cheche katika Ligi Kuu Bara baada ya kutoka sare ya bila
kufungana dhidi ya Lipuli ya Iringa.
Mechi hiyo
kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa ilikuwa ni vuta nikuvute na hadi mwisho
hakukuwa na mshindi.
Kwa sare
hiyo, Azam FC imebaki na pointi 35 baada ya kucheza 19.
Hiyo
inawafanya waendelee kubaki katika nafasi ya nne, huku wakizidiwa pointi mbili
na Yanga walio katika nafasi ya pili.
Yanga iko
katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 37 na Simba ndiyo vinara wakiwa na 42.








0 COMMENTS:
Post a Comment