FULL TIME
Dk ya 90 + 2: Mwamuzi anamaliza mchezo.
Dk ya 90: Zinaongezwa dakika mbili.
Dk ya 89: Mashabiki wa Simba wanashangilia kwa nguvu.
Dk ya 87: Simba wanafanya shambulizi kali, Gyan anaumalizia mpira kwa shuti la mguu wa kulia, Simba wanaongoza kwa mabao matano.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 84: Ndikumana anapewa kadi ya pili ya njano.
Dk ya 82: Nyoni anapiga faulo inajaa wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 82: Simba wanapata faulo karibu na lango, wachezaji wa mabo wanamzonga mwamuzi wakilalamika.
Laudit Mavugo anaingia kuchukua nafasi ya Okwi ambaye ameshindwa kurejea uwanjani.
Dk ya 78: Mchezo unaendelea, Okwi yupo nje akitibiwa. Mavugo anapasha misuli.
Dk ya 76: Okwi anatoka uwanjani akichechemea.
Dk ya 74: Simba wanapata kona, Okwi yupo chini ameumia ndani ya eneo la 18.
Dk ya 73: Simba wanaonyesha soka zuri.
Ismail Ally anaingia anatoka Emmanuel.
Kichuya anampa pasi nzuri Muzamiru Yasini ambaye naye anampa Okwi, anapiga shuti linaingia wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 68: Simba wanapata kona, Simba wanakosa nafasi ya wazi. Shuti la Kichuya linapanguliwa na kipa.
Dk ya 66: Mbao wanashambulia lango la Simba lakini shuti linatoka nje.
Dk ya 61: Okwi yupo chii, ameumia anapatiwa matibabu.
Dk ya 57: Ibrahim Njohole anaenda benchi.
Dk ya 55: Emmanuel wa Mbao analambwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Nyoni.
Dk ya 54: Nyoni wa Simba anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.
Dk ya 52: Simba wanapiga faulo fupi lakini inaokolewa.
Dakika ya 51: Mbao wanafanay amabdiliko, James Msuva anatoka, anaingia Rajesh Kotecha.
Dk ya 48: Kapombe yupo chini ameumia, mchezo umesimama.
Dk ya 48: Kichuya anautoa mpira unakuwa wa kurushwa.
Dk ya 46: Okwi anachezewa faulo na Yusuph Ndikumana, mwamuzi anapa kadi ya njano Ndikumana.
Kipindi cha pili kimeanza.
Mapumziko
Dk ya 45 + 2: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.
Dk ya 45 + 1: Habib Kiyombo anamiliki mpira lakini anakosa mtu wa kumsaidia.
Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza, mchezo unaendelea.
Dk ya 45: Mchezo umesimama kwa muda, Okwi yupo chini.
Dk ya 44: Okwi anaanguka ndani ya eneo la 18, Okwi yupo chini lakini mwamuzi anapeta.
Penalti anaipatia Simba bao la pili. Shangwe zinaongezeka kwa mashabiki wa Simba.
Okwi anapiga GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
David Mwasa amepata kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Okwi.
Dk ya 40: Penaltiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Simba wanapata penalti.
Dk ya 38: Simba wapo mbele kwa bao 1-0.
Simba wanapata bao la kwanza , mfungaji ni Kichuya akipata pasi kutoka kwa Okwi.
Dk ya 37: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk 36: Kapombe anapiga krosi lakini haina faida.
Dk ya 35: Simba wanamiliki mpira.
Dk ya 32: Gyan anapiga shuti linatoka nje kidogo ya lango.
Dk ya 31: Simba wanamtoa Said Ndemla, anaingia Mzamiru Yassin.
Dk ya 30 Simba wanapiga pasi kadhaa.
Dk ya 29: Mbao wanaingia na mpira lakini hakuna mmaliziaji.
Dk ya 27: Mbao wanapata kona, ilipigwa krosi okaokolewa.
Dk ya 24: Kichuya anapiga lakini Mbao wanaokoa.
Dk ya 23: Simba wanafanya shambulizi inakuwa kona.
Dk ya 22: Okwi anapata nafasi lakini walinzi wa Mbao wanamuwahi.
Dk ya 18: Mbao wameonyesha soka zuri. Simba wanaonyesha utulivu.
Dk ya 17: Nyoni anaupoka mpira anapigiana pasi na Kwasi na Gyan.
Dk ya 15: Mbao wanamiliki mpira kwa dakika mbili sasa.
Dk ya 10: Kipa wa Mbao anapewa kadi ya njano kutokana na kuchelewesha kuanza mpira.
Dk ya 8: Ndemla anapiga shuti lakini mpira unatoka.
Dk ya 5: Simba wanaanza kucheza kwa kuelewana.
Dk ya 1: Timu zote zinasomana.
Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha wa Mbao alishindwa kuheshimu mpinzani wake. Yeye pamoja na Mwenyekiti wao waliidharau sana Simba na kusema leo watawafunga na kuandika historia nyingine. Kilichotokea ni kweli Simba wamewaandikia historia ya wao kufungwa goli 5 bila kwenye Ligi. Haijawahi kuwatokea tangu Mbao imeanzishwa. Simba ni timu kubwa kubali usikubali. Poleni sana Mbao.
ReplyDeleteUzuri moja Simba alitulia bila tambo zisizo na maana na akafanya kweli.
ReplyDeleteSimba wameonesha kuwa wao ni ni timu kubwa
ReplyDeleteMpira ulitulia sana, licha ya Mbao kuwasumbua dk 30 za mwanzo kwa wachezaji wake akina Njohole, Maganga James Msuva na Habibu Kiyombo kuisumbua sana Simba.
ReplyDeleteKipindi cha pili walibadilika na kucheza soka tunayoitaka Simba na kuwapoteza kabisa Mbao FC, hongereni sana wachezaji na makocha wote. Simba OOOOOOOOOOOOOOOOOOOYEEEEEEEEEEEEEEEEE
Nimeamini mdomo unaponza, naona historia imewageukia wenyewe kwa kufungwa bao nyingi, tofauti na matarajio yao.
ReplyDelete