Na George Mganga
Simba imeendeleza ubabe katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuipa dozi nene Mbao FC jioni ya leo kwa mabao 5-0, mchezo ukipigwa kwenye Dimba la Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao Simba waliutawala kwa asilimia kubwa, ulianza kutikisa nyavu zake katika dakika ya 37 kupitia Shiza Kichuya, na dakika chache baadaye Emmanuel Okwi alifunga bao la pili kwa njia ya penati, baada ya kuchezewa faulo ikiwa ni dakika ya 41.
Mpaka dakika 45 za awali zinamalizika, Simba walikuwa kifua mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza huku Simba wakionesha uchu wa kufunga zaidi, ambapo 69, Emmanuel Okwi alifunga tena bao, na kufikisha mabao mawili kwenye mchezo huo.
Na katika dakika ya 82, Erasto Nyoni aliongeza bao la 3, na baadaye kuelekea mwishoni mwa mchezaji, Nicoulous Gyan akapigilia msumari wa mwisho, kwa kufunga bao la 5.
Mpaka dakika 90 zinamaliza, Simba SC 5-0 Mbao FC.
Simba walistahili kupewa penati ya pili baada ya beki wa Mbao kumchezea vibaya Okwi kwa mara ya pili. Refa akaachia lakini sio sahihi. Alitakiwa atende haki kwa kutoa adhabu inayostahili kosa lile.
ReplyDelete