FULL TIME: YANGA IMEIONDOSHA MAJIMAJI KOMBE LA SHIRIKISHO KWA USHINDI WA MABAO 2-1
Na George Mganga
5' Buswita anachezewa faulo, mpira unapigwa kuelekea lango la Majimaji
6' Hassan Kessy anachezewa mazambi, na faulo inachezwa tena kuelekea Majimaji FC
9' Ibrahim Ajibu anafanya kazi safi kwa kupiga krosi langoni mwa Majimaji lakini mabeki wanaokoa
10' Mpaka sasa matokeo ni 0-0
13' Faulo inapigwa tena kuelekea Majimaji baada ya faulo
14' Kona inapigwa kuelekea Yanga, inapigwa lakini mabeki wanaokoa
14' Majimaji wanafanya shambulio lakini umahiri wa Youthe Rostand anadaka mpira
15' Bonaventure analisakama lango la Yanga lakini mwamuzi wa pembeni anasema ni offside
19' Faulo inapihwa na Ajibu kuelekea Majimaji, kushoto wa Uwanja, anapiga lakini kipa anaipangua na kuwa kona
21' Kona imepigwa lakini mabeki wa Yanga wanaibabatiza na kuwa goal kick
21' Bonaventure anachezewa faulo na mpira unapigwa kuelekea lango la Yanga
24' Mwinyi Haji anautoa mpira na unarushwa kuelekea lango la Yanga
24' Hassan anaupiga kichwa mpira uliopigwa na Peter Mapunda na kwenda nje, kona inapigwa lakini mabeki wa Yanga wanaokoa
26' Hatarii katika lango la Majimaji inatokea piga nikupige lakini mlinda mlango wa Majimaji anaokoa
27' Bonaventure anapiga shuti hafifu lakini linakuwa rahisi kwa Rostand kulidaka
28' Goli Kiki, mpira unapigwa kuelekea lango la Yanga, matokeo bado ni 0-0
29' Mwinyi Haji anapiga krosi kushoto mwa uwanja lakini mabeki wa Majimaji wanaokoa
31' Hassan Kessy anapiga free kiki lakini inaondolewa langoni mwa Majimaji na mabeki kwa kichwa
32' Goli kiki upande wa Yanga
33' Mapunda anapata nafasi ya kufunga lakini Mwamuzi wa pembeni anasema ni offside
34' Hatarii katika lango la Yanga baada ya Mapunda kubabatizana na Rostand na kupelekea kushindwa kufunga bao la kwanza
36' Pato Ngonyani anapewa kadi ya njano baada ya kucheza mazambi
38' Said Makapu anaubabatiza mpira na unatoka, sasa ni kona kwa Majimaji
39' Marcel anapiga kona mbovu ambayo inaokolewa na beki ya Yanga
40' Gooooli, Pius Biswita anafunga goli la kuongoza kwa njia ya kichwa baada ya krosi safi ya Mwinyi haji na kuweka bao la kwanza kwa Yanga. sasa Yanga ni 1 na Majimaji ni 0.
43' Haji Mwinyi anapiga krosi safi kuelekea lango la Majimaji lakini Yanga wanaokoa, zimesalia dakika 2 mpira uwe mapumziko.
45+' Dakika 3 zimeongezwa mpira uwe mapumziko, matokeo ni 0-1
45+ Mpira unarushwa kuelekea lango la Yanga baada ya wachezaji wa Majimaji kuutoa nje
Dakika 45 zimemalizika, Yanga wanaenda kifua mbele kwa bao 1-0 likifungwa na Buswita
49' Yanga wanapata kona ya kwanza kipindi cha pili kuafuatia golikipa wa Majimaji kuutoa mpira nje ulipogwa na Ajib
51' Offside langoni mwa Yanga baada ya mwamuzi wa pembeni kuumnyoshea kibendera Mapunda aliyekuwa anashambulia
57' Gooli, Emmanuel Martin anaifungia Yanga bao la kwanza kwa njia ya kichwa, sasa Yanga wako mbele kwa bao 2-0
61' Gooli, jafar Mohammed anaipatia Majimaji bao la kwanza
69' Mpira unarushwa kuelekea lango la Majimaji, sasa umetoka na unalekezwa tena lango la Yanga, matokeo ni 1-2
71' Yanga wanafanya mabidiliko, anatoka Rafael Daud na nafasi yake inachukuliwa na Yusuph Mhilu
72' Inapigwa kona kuelekea lango la Yanga lakini kipa Rostand anadaka mpira
72' Nahodha wa Majimaji, Hassan Hamis anapewa kadi ya njano baada ya kumfanyia mazambi Yusuph Mhilu, sasa ni free kick inapigwa na Ajibu
73' Faulo inapigwa lakini inaokolewa
76' Mpira umesimama kidogo baada ya wachezaji wa Majimaji kugongana
77' Zimesalia dakika 13 mchezo kumalizika
80' Peter Mapunda anaotea tena, Majimaji wanajitahidi kushambulia lango la Yanga wakitafuta bao la kuswazisha
81' Dakika 9 zimesalia, matokeo bado ni 2-1, Yanga wanaongoza
83' Hassan Kessy anapewa kadi ya njano, sasa ni faulo inapigwa kuelekea lango la Yanga.
84' Imepigwa lakini inakwenda nje
84' Paul Lyungu anaingia kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la kwanza kwa Majimaji, Jaffar Mohammed
86' Pato Ngonyani anaenda kugangwa nje baada ya kuumia
87' Emmanuel Martin anatoka nje, nafasi yake anachukua Geoffrey Mashiuya, matokeo bado ni 2-1
90+ Dakika 3 zimeongezwa mpira umalizike
90+ Sekunde tu zimesalia mpira umalizike
90+ Rostand amelala chini baada ya kuumia, na mpira umesimama kwa muda huku wachezaji wa Majimaji wakimlalamikia Mwamuzi kuwa anapoteza muda
Na mpira umekwisha, Yanga imeibuka mshindi wa mabao 2-1, na sasa inaingia 8 bora ya robo fainali ya Azam Sports Federation CUP.
0 COMMENTS:
Post a Comment