February 25, 2018


Na George Mganga

Manchester inashuka dimbani masaa mawili yajayo katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza kuchuana na Chelsea, mechi ikichezwa kwenye dimba la Old Trafford.

United iliyo na alama 56 katika msimamo wa ligi, italazimika kushinda ili kurejea nafasi ya pili na kuindoa Liverpool iliyo na ponti 57 baada ya kushinda mchezo wake jana dhidi ya West Ham.

Faida kubwa wanayo Liverpool hivi sasa ni mabao mengi ya kufunga, tofauti na Manchester United iliyo na machache.

Chelsea nayo itafikisha alama 56 endapo itashinda leo, lakini itasalia nafasi ileile ya 4 kutokana na uhaba wa mabao ya kufunga yaliyo tofauti na United ambayo ina mengi.

Mechi hii itaanza majira ya saa 11:05 leo jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic