February 24, 2018



Mechi za Ligi Kuu Uingereza zinaendelea tena Jumamosi ya leo kwa viwanja kadhaa.

Katika Dimba la Anfield, Liverpool watakuwa wenyeji dhidi ya West Ham United, mchezo ambao utakuwa una umuhimu mkubwa kwa Liverpool kuzidi kupaa juu ya msimamo wa Ligi.

Liverpool itasonga mpaka nafasi ya pili hii leo endapo itaibuka na ushindi, na kuwa mbele kwa alama 1 dhidi ya Manchester United iliyo nafasi ya pili.

Manchester United ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 56, Liverpool wao wakiwa na 54 na timu zote zimecheza michezo sawa.

Na kama Liverpool itashinda, na katika mchezo utakaofuata Manchester United ikapoteza, Liverpool itakuwa ishajitengenezea mazingira ya kufukuzana na Manchester City walio juu ya msimamo kwa alama 72.

Manchester wao watakuwa na kibarua kigumu kesho katika Uwanja wa Old Trafford, kwa kuikaribisha Chelsea.

Ratiba ya mechi za Ligi kwa ujumla hii hapa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic