Ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza mechi nne na kutoka suluhu mara moja katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar imedai ni upepo mbaya umewakumba ila wanajipanga kufanya vizuri.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema hakuna shida yoyote kwao wala wachezaji bali ni upepo mbaya umewapitia ila mambo yatakaa sawa tu.
“Hakuna tatizo lolote, bali huku kufungwa ni upepo tu mbaya umetukumba ila tunaamini mambo yatakaa sawa tu,” alisema Kifaru.
Kifaru ameendelea kusisitiza kwamba wana matumaini makubwa ya kurejea katika mwendo wao na kuanza kufanya vizuri tena.
0 COMMENTS:
Post a Comment