SALAH ATAMBA KUTWAA TAJI HILI AKIWA NA LIVERPOOL MSIMU HUU
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah, amesema ndoto zake ndani ya Liverpool msimu huu ni kutwaa ubingwa akiwa na timu hiyo.
Salah ambaye amekuwa msaada mkubwa wa majogoo hao, mpaka sasa ameshafunga jumla ya mabao 22 katika mechi 26 za Ligi Kuu Uingereza.
"Nimekuja hapa kwa ajili ya kushinda mataji. Naweza kuwaambia mashabiki kuwa, tutajitahidi kwa asilimia 100 kadri ya uwezo wetu, walau tuweze kushinda chochote klabuni" alisema Salah.
Liverpool inaweza kupanda hadi nafasi ya pili hii leo endapo tu itaibuka na ushindi katika mchezo wake dhidi ya West Ham United, mechi ambayo itachezwa katika Uwanja wa Anfield.
0 COMMENTS:
Post a Comment