February 28, 2018


Real Madrid imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Espanyol katika Dimba la RCDE usiku wa leo katika mchezo wa La Liga.

Mechi hiyo iliyokuwa ilichukua takribani dakika 90+ kutikiswa kwa nyavu zake, zikiwa zimeongeza dakika 3, Gerard Moreno alifunga goli ambalo limemaliza mchezo huo kwa matokeo hayo.

Madrid walikuwa dimbani bila uwepo wa Cristiano Ronaldo, sasa inakuwa katika wakati mgumu wa kuwafukuzia wapinzani wao Barcelona walio na alama 65 huku Madrid akiwa na 51.

Pamoja na hayo, Kocha Zinedine Zidane anazidi kujiwekea mazingira magumu ya kuendelea kusalia kikosini hapo msimu ujao kutokana na matokeo kutokuwa mazuri kwenye ligi msimu huu.


 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic