February 24, 2018



Na George Mganga

Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho siku ya kesho, kikosi cha Majimaji kitakuwa na ukosefu wa wachezaji 7 watakaoikabili Yanga.

Kocha wa timu hiyo, Habibu Kondo, amesema timu hiyo itawakosa jumla ya wachezaji saba, na sasa watalazimika kutumia wa kikosi cha pili ili waweze kupambana.

Akizungumza na ripota wa Saleh Jembe, Kondo amesema wachezaji hao wamepumzishwa kutokana na masuala mbalimbali ya kinidhamu kuwakabili.

"Itatubidi tuingize wachezaji watano wa kikosi cha pili, sababu katika kile cha kwanza, jumla ya wachezaji saba hawatokuwepo" alisema Kondo.

Kondo amewasihi mashabiki wa timu hiyo, kujitikeza kwa wingi uwanjani ili kuipa hamasa timu yao itakapoikabili Yanga kesho katika Uwanja wao wa nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic