WENGER ASEMA MANCHESTER IMEFANIKIWA KUTOKANA NA MATUMIZI MABOVU YA FEDHA, NA SI GUARDIOLA
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ameeleza yake ya moyoni kuhusiana na namna anavykiona kikosi cha Manchester City pamoja na Pep Guardiola kuelekea fainali ya Carabao Cup.
Wenger amesema kikosi cha Manchester City kimekuwa bora kutokana na aina ya wachezaji waliosajiliwa na si uwezo wa Pep Guardiola.
Kauli hiyo ya Wenger imekuja ikiwa ni siku moja tu ya leo imesalia kuelekea mchezo wa fainali ya Carabo Cup dhidi ya City, itakayochezwa katika Uwanja wa Wembley, Uingereza.
Wenger ameeleza kuwa mpira wa dunia ya sasa umebadilika kutokana na usajili wa wachezaji bora unaofanya na vilabu.
Pia ameongezea kwa kusema kuwa Guardiola aliifundisha Barcelona ambayo mpaka sasa ni timu bora barani Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment