YANGA YAKWEA PIPA KUELEKEA SONGEA, TAYARI KUWAKABILI MAJIMAJI
Na George Mganga
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo kuelekea mkoani Ruvuma, wilaya ya Songea, kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji FC.
Yanga itakuwa mgeni katika mchezo mhuo utakaopigwa majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Majimaji uliopo mjini Songea.
Ikumbukwe Yanga ilifuzu kuendelea na mashindano baada ya kuifunga Ihefu kwa jumla ya matuta 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo wa kesho, timu itakayoshinda itaungana na Njombe Mji FC kwenye hatua ya 8 bora, ambayo ilifuzu baada ya kuitoa Mbao FC ya jijini Mwanza.
TUJIFUNZE TIMU ZA WENZETU WANAVYOVAA... HATUWAONI BARCA MAN U CHELSEA WAKISAFIRI?????
ReplyDelete