Kocha Pierre Lechantre amesisitiza wachezaji wake kuuchezea mpira zaidi lakini kwa malengo.
Katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo, Lechantre ameoneysha kusisitiza suala la wachezaji wake kuucheza mpira zaidi.
Kocha huyo raia wa Ufaransa, ameonyesha anataka soka la kushambulia zaidi na kujiamini ili kuwapa wapinzani wakati mgumu muda mwingi wa mchezo.
Mara kadhaa alikuwa anasisitiza wachezaji kujiamini lakini akawasisitiza zaidi kutokaa na mpira mguuni muda mwingi.
Kikosi cha Simba leo kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni kujiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Ruvu Shooting.
Simba inajiandaa kuivaa Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumapili.
0 COMMENTS:
Post a Comment