Kikosi cha Simba leo kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni kujiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Ruvu Shooting.
Chini ya Kocha Pierre Lechantre ameendelea kuwafua wachezaji wake kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Simba inajiandaa kuivaa Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumapili.
Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa Shooting walionyesha soka safi na la kuvutia wakati wakilala kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment