February 3, 2018




FULL TIME
KADI Dk 90+3, Gadiel analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda akiwa amekusudia


DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 90 sasa, ni miujiza tu itaifanya Lipuli kusawazisha mabao kwa kuwa hawana mipango madhubuti kuhakikisha wanasawazisha
Dk 88, Gadiel Michael analala na kuokoa dhidi ya Busungu, inakuwa kona, inachongwa inaokolewa. Wachezaji Lipuli wanalalamika Tshishimbi alishika, mwamuzi anasema cheza
SUB Dk 86, Juma Mahadhi anaingia nafasi ya Raphael anayekwenda benchi
Dk 83 Chirwa tena anaingia vizuri, krosi yake inazuiliwa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa, unakuwa wa kurushwa


SUB Dk 81, Mwashiuya anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Maka Edward
Dk 80 sasa, kipa Kabwili wa Yanga yuko chini baada ya kugongana na Salamba, anapatiwa matibabu
SUB Dk 78, Jerome Lambele anaingia kuchukua nafasi ya Mnyate upande wa Lipuli
Dk 75, krosi nzuri ya Busungu ambaye anamsumbua sana Kessy, inaokolewa
Dk 73 Busungu anamtoka Kessy na kupiga krosi safi kabisa, lakini Zawadi anaruka legevu na kuupiga juu ya lango, goal kick
SUB Dk 71 Zawadi Mawia anaingia upande wa Lipuli, Mussa Nampaka anakwenda kupumzika
Dk 70 sasa, hakuna matumaini kwamba Lipuli watasawazisha kwa kuwa hawana mipango bora


SUB Dk 68 Lipuli wanamatoa Kalihe na nafasi yake inachukuliwa na Tola Mangonela
Dk 67, Kalihe anaachia mkwaju mkali, unamtoka Kabwili lakini mabeki Yanga wanaokoa
Dk 66, Chirwa tena, mkwaju mkali unapanguliwa na kipa
KADI Dk 63, Gadiel anawachambua mabeki wa Lipuli, anawekwa chini, mwamuzi anasema ni adhabu na KADI YA NJANO inakwenda kwa Martin Kazila
Dk 60 Chirwa anawatoka tena Lipuli, krosi yake safi, inakuwa kona baada ya kuokolewa, inachongwa wanaokoa
Dk 59 Yondani yuko chini anatibiwa baada ya kugongwa na mpira 


Dk 58, Lipuli wanalisakama lango la Yanga, wanapata kona, inachongwa lakini Yanga wanaondosha
GOOOOOOOOO Dk 55, Yanga wanapiga kaunta atak ya uhakika ni Tshishimbi, Buswita, Chirwa anapiga krosi inamkuta Buswita ambaye anamchambua kipa na kuandika bao safi la pili la Yanga leo KADI Dk 54, Mwashiuya analambwa kadi ya njano kutokana na kumchezea kindava Kalihe 
Dk 53 Yanga wanapata kona baada ya BUswita kuachia mkwaju uliozuliwa, inachongwa, goal kick
Dk 53, shuti la Busungu linagonga mwamba wa Yanga na kurudi uwanjani


Dk 52 krosi nzuri ya Tshishimbi, Buswita yeye na kipa anampa mkononi
Dk 49 Mwashiuya anapiga kanzu bombaa kabisa, anaachia mkwaju mkali ndani ya 18, goal kick
Dk 48, Busungu anaachia mkwaju mkali kabisa, Kabwili anapangua kwa ustadi mkubwa
Dk 47, Salamba anaachia mkwaju mkali, Kabwili anapangua vizuri lakini mwamuzi anasema ilikuwa ni offside tayari
Dk 46, Lipuli wanajaribu mara ya pili lakini bado inaonekana hawako makini
Dk 45, Lipuli wanaanza kwa kasi kabisa hapa lakini Yanga wako makini

MAPUMZIKO
KADI -Salamba analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava


DAKIKA 10 ZA NYONGEZA
Dk 45, krosi safi, Salamba anapiga kichwa vizuri lakini goal kick
Dk 42, krosi nzuri ya Chirwa, Martin anaruka na kupiga kichwa, goal kick
KADI Dk 41, Kabwili analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda kwa makusudi


Dk 40 mkwaju wa adhabu unachongwa na Salamba, lakini faulo dhaiiifuuuu, goal kick
Dk 38 sasa, Mwashiuya anafanya madhambi nje kidogo ya boksi la Yanga. Naye yuko chini, wote wanatibiwa
Dk 34, nafasi nzuri kwa Yanga lakini Raphael anaachia shuti dhaifu kabisa
Dk 30, Shambulizi kali la kwanza la Lipuli, mkwaju mkali Kabwili anaokoa lakini Mnyate anapiga shuti kuuubwa, goal kick
DK 29, Mpira ulisimama, mchezaji Lipuli akilalama kupigwa kiwiko


Dk 26 Martin anaachia mwaju mkali kwelikweli, Aghaton anapangua na kuwa kona, inachongwa na Kessy, Tshishimbi anapiga kichwa, goal kick
Dk 24,Kona safi inachongwa, Yanga wanaokoa inakuwa kona tena lakini Lipuli wanafanya madhambi tena na Erick Onoka, mwamuzi wa leo, anasema ni faulo
DK 22, Lipuli FC nao wanapata kona, inachongwa na Mganga, lakini imezuiwa kwa kuwa mwamuzi anazuia maana kipa Kabwili yuko chini pale
GOOOOOOOOOO Dk 19 kona safi ya Kessy, Martin anaipiga kichwa, kipa anapangua na mpira unamkuta Tshishimbi akiwa na nyavu anaachia shuti kali la makusudi na kuandika bao safi la kwanza la Yanga


Dk 18, Chirwa anaingia vizuri, Lipuli wanatoa na kuwa kona
SUB Dk 17, Yanga wanamtoa Rostand ambaye ameshindwa kuendelea na nafasi yake inachukuliwa na kinda Ramadhani Kabwili
Dk 14 sasa, zimepita dakika 2, kipa wa Yanga yuko chini akipatiwa matibabu
Dk 10 sasa, bado hakuna mashambulizi makali sana kwa kuwa mpira zaidi uko katikati ya uwanja
DK 8, Rostand anatoka na kudaka vizuri kabisa krosi nzuri la Salamba ambaye anaonekana kuwa mwiba katika ngome ya Yanga


Dk 6 Yanga wanaingia vizuri tena, krosi nzuri ya Gadiel lakini kipa wa Lipuli, anawahi
Dk 3, Lipuli wanaingia vizuri katika lango la Yanga lakini Jamal Mnyate anadhibitiwa vizuri
Dk 1, Mechi imeanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui FC lakini ni goal kick.

Hali ya hewa ni joto kali, si baridi kama Iringa ilivyozoeleka.


KIKOSI CHA LIPULI LEO

1. Agathon Anthon
 2. Steven Mganga
3. Ally Mtoni
4. Martin Kazila
5. Joseph Owino
 6. Novatus Lufunga
7. Seif Rashid 
8. Mussa Nampaka
9. Malimi Busungu
10. Adam Salamba
11.Jamal Mnyate

4 COMMENTS:

  1. Hongera Yanga kwa ushindi mzuri wa ugenini. Timu ilicheza vizuri hasa Chirwa.

    ReplyDelete
  2. Mkubwa blog yako isiwe kwaajili ya simba na yanga tu. Toa updates za timu zote zinazoshiriki ligi kuu. Wengine tunategemea kupata habari kwa njia ya mtandao hivyo usibague. Toa details za timu zote bila ya kujali ukubwa wa timu. Ni ushauri tu, otherwise unaweza kufanya upendavyo tu.

    ReplyDelete
  3. Azam walicheza jana kama sikosei, lakini matokeo hayapo mtandaoni kupitia blog yako na hata nyingine. Ifanye blog kuwa one size fits all.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic