February 26, 2018



Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amefunguka kuwa kuna sababu kubwa ya benchi la ufundi la timu hiyo kumtumia kipa Ramadhani Kabwili badala ya Mcameroon, Youthe Rostand kwa kuwa amekuwa akifanya makosa ya kizembe yanayojirudia kila wakati.

 Mzee Akilimali ameyasema hayo kufuatia kipa huyo kufungisha bao kwa uzembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis ya Shelisheli kwenye mchezo wa marudiano uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 wakati bao lingine akifungisha katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba, mfungaji akiwa ni Shiza Kichuya.

Mzee Akilimali alisema kuwa haoni sababu ya benchi la ufundi linaloongozwa na Mzambia, George Lwandamina kuendelea kumtumia kipa huyo katika mechi zake kwa kuwa amekuwa akigharimu timu kila wakati jambo ambalo linawapa wakati mgumu.


"Kiukweli msimu huu hatujapata mbadala wa makipa wetu walioondoka Yanga kama Deogratius Munishi 'Dida', Ally Mustapha 'Barthez' ambao walikuwa bora zaidi ya huyu kipa wa kigeni ambaye tupo naye hivi sasa, amekuwa akifanya uzembe mara nyingi na kuigharimu timu.

"Nadhani kuna haja ya  benchi la ufundi kumuangalia yule mtoto Kabwili aliyetoka Serengeti Boys kuliko kuendelea kumtumia yule, sijui yule kipa  mwingine (Beno Kakolanya) nasikia kwamba ana matatizo na uongozi, hayo siwezi kuingilia lakini huyu mgeni hatufai kwa kweli," alisema Mzee Akilimali. 

SOURCE: CHAMPIONI


1 COMMENTS:

  1. Ni maoni yake Mzee wetu hakuna ubaya yeye kutoa maoni yake na kushauri vile anavyoona yeye inafaa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic