February 26, 2018



Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, amemwongezea majukumu mapya kiungo wake mkabaji, Jonas Mkude ambayo anapaswa kufanya pindi anapokuwa uwanjani.

Kuanzia sasa Mkude anatakiwa kuwa na jicho la mwewe la kuwaangalia washambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi na John Bocco wamekaaje na kuwapigia mipira mirefu ambayo itawasaidia kufika katika eneo la wapinzani wao kwa haraka zaidi.

Lakini pia mbali na kufanya hivyo, Mkude ametakiwa kuhakikisha anakuwa na uwezo mkubwa wa kuisaidia safu ya ulinzi kujilinda pindi timu hiyo inaposhambuliwa kwa zaidi.

Mkude amesema kuwa hivi sasa anayafanyia kazi maelekezo hayo kwa nguvu zake zote.

“Kuna mambo mengi ambayo kocha anayaona kutoka kwangu ambayo natakiwa kuyafanya ili niweze kuwa bora zaidi, kwa hiyo ninapambana ili niweze kuyafikia.

“Kuna majukumu ambayo amenipatia na sasa ninayafanyia kazi, baadhi ni kuhakikisha nakuwa vizuri katika kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza lakini pia kujilinda pindi tunapokuwa tunashambuliwa zaidi,” alisema Mkude.


SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic