February 24, 2018


Kocha wa zamani wa FC. Barcelona na Manchester City kwa sasa, Pep Guardiola, ameshitakiwa na Chama cha Soka Uingereza (FA), kwa kosa la kuvaa riboni yenye ujumbe wa kisiasa.

Guardiola alivaa riboni hiyo katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic, ambao aliangukia pua kwa kulala kwa bao 1-0 na kutupwa nje ya mashindano.

Taarifa zinaeleza kuwa Guardiola alivaa ujumbe huo kwa lengo la kuwasapoti wanasiasa wa Kikatalunya waliopo nchini Spain waliofungwa gerezani.

Kwa mujibu wa FA, sheria na taratibu zao katika soka haziruhusu mpira kuingiliana na masuala ya siasa hivyo wameamua kuchukua hatua hiyo Kocha Guardiola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic