February 4, 2018



Pamoja na juhudi kuu alizokuwa akizifanya, Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameshindwa kutimiza ndoto yake ya kurejea Ligi Kuu Bara.

Kikosi chake cha Dodoma FC kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African lakini timu inaendelea kubaki Ligi Daraja la Kwanza.

Hiyo inatokana na ushindi wa Biashara Mara dhidi ya Transit Camp ambao umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 30 na Alliance imefikisha pointi 28 baada ya kuitwanga JKT Oljoro.


Ushindi wa leo umeifanya Dodoma FC kufikisha pointi28 pia lakini wastani wake wa mabao ya kufunga na kufungwa ndiyo yanaibakisha Ligi Daraja la Kwanza.

1 COMMENTS:

  1. Ila maneno mengi wakati mwengine yasiofuatana na vitendo huleta kichefu chefu. Julio alitoa maneno ya shombo juu ya kocha mrundi wa Simba aliekuwa akiisimamia timu kabla ya kuja kocha mkuu mfaransa. Julio alijipiga kifua kuwa yeye ndie mwenye uwezo wa kuifundisha Simba na sio mrundi lakini Mrundi alifanya kazi na kuzungumza kwa vitendo kwa muda mchache aliyosimamia timu na hata wachezaji wenyewe wa Simba ukiwauliza watakwambia kuwa mrundi ni kocha. Ni kocha mwenye uwezo wa kuleta tofauti kwa timu na mchezaji mmoja mmoja. Pongezi kwa viongozi wa Simba kwa kuamua sio tu kubadilisha gia angani bali kubadilisha rubani angani jamabo ambalo wadau karibu wote walionekana kupingana na maamuzi yale lakini actions always sounds louder than just empty talking. Simba sasa ina bench imara la ufundi kiasi cha kushangaza na hii inaonesha jinsi gani viongozi wa Simba walivyo serious na wanachotaka kukifanya kwa timu na wanamsimbazi. Viongozi wa namna hii ilikuwa vigumu kumuachia kocha kama Omog kuendelea kuwapa pressure kila timu yao ikicheza. Inaonekana watanzania wengi ni watu wa kuridhika na kidogo nawanachikipata au kutopata kabisa na ni watu waliotawaliwa na woga wa kuchukua maamuzi hata kama hali waliyonayo ni ya mashaka na tabu. Kurudi kwa Julio na Dodoma Afc Ile timu kwa kipindi alichokaa Julio kama ingelikuwa chini ya Masoud Djuma sasa tunavyozungumza ingekuwa ipo ligi kuu na huo ndio ukweli. Ni wape tu credit viongozi wa Simba na hasa Mohamed Mo kwani kuonesha hisia zake za kukerwa na matokeo ya kombe la FA ilikuwa ndio chachu na chanzo cha kuchukua maamuzi ya kumtimua Omog na watu wengi tu walimvurumishia makombora ya kumbeza, japo simba bado haijachukuwa ubingwa lakini timu inaonesha mabadiliko makubwa tangu Omog kaondoka, utaona kabisa vijana wanatafuta kitu fulani kwa juhudi kubwa kabisa na hiyo yote inatokana na mabadiliko yanayotokana na mafundisho kutoka bench la ufundi .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic