February 4, 2018




Biashara Mara imekuwa timu ya tano kupanda Ligi Kuu Bara na kuamsha shamgwe mkoani humo ambako walikuwa wakitaka kwa hamu kubwa kuiona ligi hiyo.

Biashara imefanikiwa kupanda baada ya kuitwanga Transit Camp kwa mabao 3-2 katika mechi kali mjini Musoma.

Ushindi huo unaifanya Biashara kufikisha pointi 30 na kubaki kileleni mwa Kundi C ikifuatiwa na Alliance.

Wenyeji Biashara walilazimika kufanya kazi ya ziada kupata mabao ya haraka baada ya timu hizo kushindwa kufungana mapema.

Timu nyingine nne zilizopanda Ligi Kuu Bara ni pamoja na JKT Ruvu iliyokuwa ya kwanza, KMC ya Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance ya Mwanza na Biashara.

Sasa imebaki timu moja inayotafutwa kukamilisha idadi ya timu sita zinazotakiwa kupanda ligi kuu msimu ujao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic