Na George Mganga
Droo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inafanyika kesho Ijumaa, Machi 2, 2018 saa 5 asubuhi, katika Makao Makuu ya Azam Tv, walipo wadhamini wa mashindano hayo.
Droo hiyo itahusisha timu nane (8) zilizofanikiwa kufuzu hatua hiyo ya Nane bora.
Timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Young Africans na Azam FC za Dar es Salaam, Singida United ya Singida, Njombe Mji ya Njombe, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Tanzania Prisons ya Mbeya, Stand United ya Shinyanga na JKT Tanzania ya Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment