Na George Mganga
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa 19 inataraji kuendelea kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya Shinyanga.
Mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi wa katikati atakuwa ni Florentina Zabron kutokea Dodoma, Mwamuzi Msaidizi namba moja atakuwa Ferdinand Chacha wa Mwanza.
Vilevile Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza, Mwamuzi wa akiba ni Gelmina Simon wa Dar es Salaam na Kamishna wa mechi anatoka Arusha, Peter Temu.
0 COMMENTS:
Post a Comment