KLOPP: SALAH NI MESSI MPYA
Baada ya kufunga mabao manne katika mchezo wa Ligi Kuu England huku Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0, Kocha Jurgen Klopp, asema mchezaji huyo anafuata nyayo za Messi.
Salah alifunga mabao hayo jana dhidi ya Watford kwenye dakika za 4, 43, 77 na 85 wakati la tanio akifunga Roberto Firmino (49').
Kutokana na kiwango alichokionesha Salah, Klopp alisema mchezaji huyo njiani kuanza kulinganishwa na Messi.
"Nadhani yuko njiani kufuata nyendo zake, sidhani kama Mo au kila mchezaji anastahili kulinganishwa na Messi, lakini Salah ni mchezaji mzuri na anaelekea huko" alisema Klopp.
2 COMMENTS:
ReplyDelete
ReplyDelete