April 10, 2019


KMC Leo watashuka Uwanja wa Namfua kumenyana na Singida United ya Felix Minziro ambaye ndiye alizipandisha daraja timu zote mbili.

KMC ipo chini ya kocha Ettiene Ndiyaragije ambaye alitwaa mikoba ya Minziro anayekutana naye leo uwanjani.

Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani na wanaamini kwa mbinu ambazo wamepewa na kocha zitawapa matokeo chanya.

"Kikosi kipo salama na morali ya wachezaji ni kubwa, tunawaheshimu wapinzani wetu na nina amini wachezaji watapambana kupata matokeo chanya," amesema Binde.

KMC ipo nafasi ya 7 baada ya kucheza michezo 30 kibindoni ina pointi 41 imeshinda michezo 9 na imepoteza michezo 7 huku ikiwa na sare 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic