December 19, 2020

 


LABDA ndilo jina lililotamkwa zaidi wiki hii. Hery Sasii. Muamuzi aliyewapa Simba penalti isiyokuwa ya halali, ikafungwa na mshambuliaji wao hatari Meddie Kagere.

Ilikuwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC. Wakati Simba wanashambulia mpira ulimgonga mshambuliaji wa KMC Hassan Kabunda ‘Ninja’ katika eneo la tumbo, muamuzi akatafsiri kuwa Kabunda ameunawa mpira. Akatenga tuta.

Sijui Sasi aliona vipi kuwa mpira umegusa mkono. Wakati mpira unapigwa na beki wa KMC kabla haujatua kwenye tumbo la Kabunda, mikono ya Hassan Kabunda ilikuwa juu. Mikono ya Kabunda ilishuka chini wakati anaosha mpira kuuondoa kwenye eneo la hatari.

 Muda wote huu wakati tukio linatokea Sasii alikuwa nyuma ya mgongo wa Kabunda. Aliona vipi kuwa mpira umegusa mkono? Anajua mwenyewe.

Kinacho muhukumu zaidi Sasii ni kuwa, penalti aliyotoa ndiyo imeamua mchezo. Ingekuwa rahisi sana kwa ‘watu kupotezea’ kama Simba wangefunga bao lingine na kushinda mbili kwa sifuri au kama KMC ingesawazisha na kupata bao lingine la ushindi.

 

 Watanzania huwa hawajali sana  matukio yasiyobadilisha matokeo. Utasikia mtu akikuambia, hata lile tuta lisingetolewa bado tungeshinda kwasababu tulifunga mabao mengine matatu. Hatuna tabia ya kufiri na kujali athari ya baadhi ya vitu vinavyotuangusha maishani. Tunapenda kujitetea kwa hoja nyepesi. Sisi bwana!

Hili la Sasii ni muendelezo wa sinema zinazoendelea kuchezwa na waamuzi wa Kitanzania katika ligi za Tanzania. Sasi huyu-huyu amewahi kuharibu mechi ya Yanga na Azam pale kwa Mkapa. 

Mechi ambayo ingeweza kuisha kwa mabao matatu kwa moja ikamalizika kwa sare tasa. Siku hiyo Sasii aliwanyima Azam mabao mawili ya halali na penalti moja kisha akawanyima yanga penalti baada ya David Molinga kukwatuliwa na Wadada katika box la azam.

Wahanga wa juzi KMC, walikuwa wahanga tena wa uamuzi mbovu walipocheza dhidi Yanga kule Mwanza. Yanga walipewa penalti isiyo halali iliyofungwa na ‘mkongomani’ Tuisila Kisinda. Yanga haohao walifaidika na maamuzi mabovu ya mwamuzi walipocheza na Gwambina kule Misungwi. Gwambina wakanyimwa bao la halali kabisa. Hukohuko kanda ya ziwa, Azam walinufaika na maamuzi mabovu ya muamuzi dhidi ya Biashara. Muamuzi akakubali bao la ‘offside’ la Ayoub Lyanga.

Haya ni matukio machache tu ninayoyakumbuka yaliyotokea katika mechi ya hizi timu tatu kubwa. Vipi kwa timu ndogo? Vipi kwa matukio ambayo siyakumbuki? Hali ya waamuzi wetu ni mbaya sana. Nini kinawakumba?

Ni swali gumu sana kulijibu ukizingatia upo nje ya fani ya uamuzi. Kutoa maoni tu inatosha. Kwanza nina wasiwasi na ukufunzi wanaofanyiwa waamuzi wetu. Haiwezekani kila siku muamuzi mmoja atende makosa yaleyale.

Haiwezekani kila siku waamuzi tofauti warudie makosa yanayofanana. Tunakubali ubinadamu upo, lakini ubinadamu gani huu wa kila siku? Makosa mengi yanatokana na uzembe tunaosingizia ni ubinadamu. Uzembe unaotokana na maandalizi mabovu.

Bado siamini kama kuna marefa wanaokubali kuhongwa katika karne ya 21. Kama watanzania zaidi ya milioni 3 wanaangalia mpira kwenye televisheni, hakuna jinsi unaweza kuwadanganya. Lazima utaumbuka tu. Bado imani yangu inaniambia marefa wetu hawajui sana wanachokifanya ndiyo maana wanakosea sana. Hoja ya kuhongwa hainiingii sana.

Mwisho kabisa tuwaelewe wenzetu walioamua kuingiza teknolojia ifanye kazi kwenye soka. Pengine huu mjadala wote usingekuwepo kama siku ile pale kwa Mkapa kungekuwa na ‘VAR’. Muamuzi angeenda tu pembeni kutazama na kupindua maamuzi yake. Sasa tuelewe kwanini wazungu wameamua kutumia mashine.

 

13 COMMENTS:

  1. Tulijua tu mtaibuka na chambuzi zenu feki mbona hujazungumzia mechi ya yanga na Simba, tatizo lenu mahaba yamezidi na tutasikia mengi Simba ikichukua nafasi yake ya uongozi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mechi IPI hivyo? Ile ya Kagere alipovuliwa hurizi na Yondani nje ya 18 akaangukia ndani na Jonisia akawapa penati?

      Delete
  2. Hivi kwa nini TFF inaishia kuvipiga faini vilabu na viongozi wao na kuwaacha wachochezi kama hawa kutokana na matamko su maandiko yao yanayohukumu su kuingilia majukumu yasiyowahusu.Je kama ingekuwa ni mahakama ndo imetoa hukumu halafu huyu mwandishi aandike hakimu aliyetoa hukumu isiyo halali amefanya jambo fulani nadhani sasa hivi angekuwa kizimbani.Ifike mahali waandishi wawe na mipaka katika kutumia kalamu zao na sio kutumia kalamu zao kuhukumu.Mbona kila siku hii blog inaandika makosa mengi tu lakini hatujaona hata siku moja mkijihukumu kwa makosa yenu japokuwa sisi wasomaji tumekuwa tukikosoa na kuwataka mjirekebishe lakini hamjali hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. Imeisha iyo tafuten nada nyengine

    ReplyDelete
  4. Kwa hili mwandishi ana hoja y msingi mno pia mm Kama mpenzi wa mpira najiulizaga kwann maamuzi mengi mabovu mara nyingi yanawanufaisha Simba na yanga t?hapa Kuna namna kwa hoja y leo inamashiko TFF waviangalie Simba na yanga inawezekana ndo hasa wanaodumaza mpira wa tz

    ReplyDelete
  5. Sawa na refa ni binadamu...wakati mwingine inaeleweka..imechambuliwa vizuri na kipenga cha mwisho...kaangalie youtube kama ulipitwa.Mbona Diego Maradona alifunga kwa mkono na sababu hiyo wakafikia chukua kombe la dunia..
    Utopolo aka matopeni aka gongowazi wako hapo walipo sababu ya penalti mbili za makosa nje ya 18...sembuse hiyo iliyotokea ndani ya 18. Hii penalti itawakera saanaaa maana inamuweka Simba katika nafasi ya kupumulia shingoni kwenu..Mkipata penalti za makosa hamuandiki... wengine wakipata kila baada ya 48 hours mnaandika..Na kesho kutwa tunategemea mtaandika kuhusu morrison ingawa hayuko Zimbambwe

    ReplyDelete
  6. Jamani wapendwa tuangalie mbele hata Kama tunasema mikia ilibebwa lkn ukweli huo mpira ulienda golini kwa KMC kwa Nia ya kutafuta goli.Siyo Kama basketball ampapo faulu ya golini kwa jirani inaletwa kwako .Refa alikosea lkn Marsha yaendelee pls Wanaume tunaangalia mbele always

    ReplyDelete
  7. 𝐖𝐚𝐚𝐦𝐮𝐳𝐢 𝐰𝐞𝐭𝐮 𝐰𝐚𝐰𝐞 𝐦𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐡𝐚𝐫𝐢𝐛𝐮 𝐬𝐨𝐤𝐚 𝐥𝐞𝐭𝐮 𝐥𝐚 𝐧𝐝𝐚𝐧𝐢 𝐥𝐢𝐧𝐚𝐥𝐨𝐥𝐞𝐭𝐚 𝐡𝐚𝐬𝐚𝐫𝐚 𝐤𝐢𝐭𝐚𝐢𝐟𝐚 𝐧𝐚 𝐤𝐢𝐦𝐚𝐭𝐚𝐢𝐟𝐚

    ReplyDelete
  8. Mwandishi,hiyo isiyokungia akilini ndio,yenyewe sasa.kuna refa laini yake simu mwezi huu imerushiwa laki tano x4 kutoka kwenye namba iliyorushiwa na mawakala tofauti yeye aliomba simu.uozo mtupu,

    ReplyDelete
  9. Mda mwingine akir zako zinaenda likizo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic