March 19, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuondolewa na Al Masry kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Uongozi wa Simba SC umesema wao ni mashujaa.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Simba wameandika kuwa wao ni mashujaa kwakuwa hawajafungwa bali wametolewa kwenye mashindano.Kauli hiyo imekuja kuafuatia Simba kwenda sare ya mabao 2-2 dhidi ya Al Masry katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam, na marudiano huko Misri ukimalizika kwa suluhu ya 0-0.

Baada ya kusema kuwa wao ni shupavu, kikosi hicho kimewaomba mashabiki waipokee timu hiyo itakapowasili jijini Dar es Salaam, ikitokea Cairo, Misri leo.
1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV