March 19, 2018


Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, jana amefikisha 'Hat-trick' ya 50 katika maisha yake ya soka.

Hat-trick hiyo ya 50 ameipata baada ya kufunga jumla ya mabao manne, Madrid ikiitwanga Girona kwa idadi ya mabao 6-3.

Katika mchezo huo uliopigwa Santiago Bernabeu, Ronaldo alifunga mabao kwenye dakika za 11, 47, 64 na 90+1 huku mengine yakifungwa na Benzema dakika ya 86 pamoja na Vazquez dakika ya 59.

Mbali na kuweka rekodi hiyo, Ronaldo sasa amebakiza mabao matatu pekee kumfikia mpinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona aliyefunga mabao 25 kwenye La Liga msimu huu wakati Ronaldo akiwa na 22.

Ronaldo amempita Luis Suarez kwenye nafasi ya pili, ambapo mpaka sasa ana mabao 21.

Msimamo wa Ligi Kuu Spain sasa unaonesha Real Madrid ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 60 ikicheza michezo 29, wakati vinara Barcelona wao wana alama 75. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic