Dak ya 3, Mechi ya Yanga vs Kagera Sugar imeanza hivi punde
Dak ya 4, haji Mwinyi anarusha mpira kuelekea lango la Kagera baada ya kutolewa, anauchukua Ajib, Ajib anapasia langoni mwa wapinzani, wanaokoa
Dak ya 5, Kagera sasa, anao Atupele Green, pasia pembeni mwa Uwanja, hatariii, Kagera wanakosa nafasi ya wazi
Dak ya 7, Rostand anaanzisha goli kiki, ni baada ya mpira kutoka nje
Dak ya 8, Buswiiiita, namna gani hapa, krosi yake inakwenda nje, ilikuwa ni pasi nzuri ya auta kutoka kwa Ajib
Dak ya 12, Matokeo ni 0-0 mpaka sasa
Dak ya 13, Hatari katika lango la Kagera hapa, Buswiita, anababatizana na mlinda mlango, anaudaka
Dak ya 14, Mpira umesimama baada ya kipa wa Kagera kuumia, Cannavaro naye anapasha nje
Dak ya 15, tayari mpira umeshaanza, kwake Kamusoko, anapiga shuti lakini linatoka nje
Dak ya 16, Offside, Kagare wanaotea, mpira unapigwa kuelekea kwao
Dak ya 18, Kibaya anapata kadi ya njano, ni ya kwanza kwenye mchezo wa leo
Dak ya 19, Faulo, kadi ya pili ya njano inaenda kwa mchezaji wa Kagera, ni baada ya kucheza faulo eneo la hatari, inapigwa langoni mwao
Dak ya 20, Ajib yuko na mpira, anapigaaa, inapiga nyavu za juu
Dak ya 21, Ngonyani naye anapata kadi ya njano baada ya kucheza mazambi, ni ya tatu sasa katika mchezo huu
Dak ya 21, Matokeo ni 0-0
Dak ya 22, Mpira umesimama, Maxime anatoa maelekezo kwa wachezaji wake
Dak ya 23, Fhaki anapiga hapa, hatari langoni mwa Yanga, namna gani mshambuliaji huyu anashindwa kutumia nafasi
Dak ya 25, Kavila anamchezea rafu Chirwa hapa, inakuwa faulo kwenda Kagera
Dak ya 25, Ally Nasoro sasa anaondoka nao kupandisha mashambulizi, anapiga pasi mkaa, anaokoa Yondani
Dak ya 26, Wanaanza Yanga eneo la nyuma, Kessy anampasia Buswita, kwake Kamusoko, Kamusoko anapiga kwake Pato lakini beki wa Kagera anautoa na mpira unakuwa wa kona
Dak ya 28, Mpira anao Kamusoko, anapasia nyuma kwake Yondani, Yanga wanajaribu kutafuta bao hapa
Dak ya 29, Emmanuel Martin, anacheza faulo, mpira unapigwa kuelekea Yanga
Dak ya 30, matokeo ni 0-0, mpaka sasa hakuna timu iliyofanya shambulizi la kutisha kwa mwenzake
Dak ya 31, Goli Kiki upande wa Yanga, unapigwa kuelekea Kagera
Dak ya 32, Kagera waanzisha goli kiki, tayari ushapigwa, faulo, unapigwa kuelekea Kagera
Dak ya 33, Mabadiliko Yanga wanafanya mapema, anatoka Pato na nafasi yake inachukuliwa na Maka
Dak ya 35, Kagera wanapata kona ya kwanza baada ya Mwinyi Haji kuutoa mpira, inapigwaaa, inapigwa kichwa na mshambuliaji wa Kagera lakini kipa Rostand anadaka
Dak ya 37, Unarushwa sasa kuelekea lango la Kagera, anao Ajib sasa, kwake Martin, unapigwa kwake Buswita, anautuliza kwa njia ya kifua lakini beki wa Kagera anaokoa
Dak ya 39, Anao sasa Ajib, unapigwa langoni, kipa anajitutumua anaupiga na mkono unakuwa wa kurushwa kuelekea langoni kwake, kidogo iwe kona
Dak ya 41, Faulo, Ajib anapiga, anapiga ya chinichini lakini mabeki wanaokoa kwa kichwa
Dak ya 41, Mpira uko mbele sasa upande wa kulia mwa uwanja wanao Yanga, beki wa Kagera anauokoa hapa, unapigwa mbele lakini Maka anautoa nje
Mpira ni mapumziko sasa, Yanga 0-0 Kagera Sugar
Dak ya 45, Kipindi cha pili kimeanza, matokeo ni 0-0
Dak ya 46, Beki wa Kagera anachezewa faulo, mpira unapigwa kuelekea langoni mwa Yanga
Dak ya 47, Hatarii langoni mwa Yanga, Atupele Green anakosa kupiga shuti nje kidogo mwa eneo la hatari, ni faulo,
Dak ya 48, Inapigwaaa, inatoka nje sentimita kadhaa tu, bahati nyingine wanaikosa Kagera Sugar,
Dak ya 50, Yanga wanaanza nyuma taraatibu, beki wa Kagera anautoa nje
Dak ya 51, Penatiiii, Yanga wanapata tuta hapa
Dak ya 51, Ajib ndiyo anapiga tuta, anapigaaa, gooooooli, Yanga wanapata bao la kwanza, sasa ni 1-0
Dak ya 53, Kagera wanaanza upya kati, wanapasiana kuelekea langoni mwa Yanga, inapigwa moja juu, kipa Rostand anaruka kama nyani anaudaka
Dak ya 55, Kagera wamezidi kuamka licha ya kufungwa bao hilo moja, wanamiliki zaidi mpira eneo la kati
Dak ya 57, Ajib sasa na mpira, piga huku pembeni lakini Kagera wanaokoa, inapigwa mbele hukuu, offside
Dak ya 59, Namna gani Kagera wanakosa tena bao hapa, ni nafasi adhimu kabisa hii ndani ya eneo la hatari mwa Yanga, mpira unakwenda nje
Dak ya 61, Kagera wanaanza mashambulizi tena, wanapasiana eneo la nyuma
Dak ya 63, Faulo inapigwa kuelekea Kagera baada ya beki wake kucheza mazambi
Dak ya 64, Yanga wanao mpira hivi sasa, Ajib anajaribu kuzunguka lakini ananyang'anywa mpira, Kamusoko anauwahi
Dak ya 65, Mpira anao Fhaki sasa, pasia kati ya uwanja huku, unarejeshwa kwake Fakhi tena, Kagera bado wanaumiliki, pigwa huku langoni mwa Yanga, offside
Dak ya 68, Kagera wanashindwa kutumia vema nafasi ya kufunga baada ya kupasiana vizuri na kuingia eneo la hatari la Yanga
Dak ya 69, Kona wanapata Yanga, ni ya nne na tano katika mchezo wa leo, Ajib anapiga lakini inaokolewa
Dak ya 70, Chirwaa, anapiga krosi moja ya hewani lakini inatoka nje
Dak ya 71, Mpira umesimaa kidogo, mchezaji wa Kagera ameumia
Dak ya 72, Omary Daga anaingia kuchuka nafasi ya Atupele Green, matokeo bado ni 1-0
Dak ya 75, Yanga wanapata kona, inapigwa na Ajib, pigwa huku Chirwa anapiga kichwa lakini inaenda pembeni, Kagera wanaokoa
Dak ya 75, Emmanuel Martiiiin, anapigaaaa, kipa wa Kagera anakuwa mahiri anaokoa
Dak ya 76, Goooooooli, Martin anaifungia Yanga bao la pili kufuatia krosi nzuri ya Obrey Chirwa, Yanga wana mabao mawili sasa na Kagera 0
Dak ya 79, Yanga wameamka sasa, wanakwenda mbele na mpira, kona! Ajib yu tayari kupiga, anaanza fupi hukuuu, kona nyingine, ni ya 7 sasa, inapigwaaaa, Kagera wanaokoa
Dak ya 81, Kagera wanapata kona pia, inapigwaaa lakini inaokolewa
Dak ya 82, Kagera wanaumiliki mpira tena, wanajaribu kutafuta bao angalau la kufutia machozi
Dak ya 83, Hatari langoni mwa Kagera, kipa anadaka, anaanza taratibu na wenzake nyuma
Dak ya 85, Kagera wanapata kona hapa, inapigwa lakini inatolewa na kuwa kona ya pili, inapigwa tena hukuu, Rostand anadaka na kutulia vizuuri kabisa
Dak ya 87, Yanga wanao sasa, Buswita, kwake Kessy, anarudisha kwa kipa wake
Dak ya 88, Yusuph Mhilu anakwenda na mpira upande wa kulia wa uwanja, anapigaa, gooooooli, Kagera wanajifunga katika harakati za kuokoa, sasa ni 3-0
Dak ya 90, Zimeongezwa dakika tatu pekee mpira umalizike
FULL TIME
Mwamuzi anapuliza kipyenga kumaliza mpira, Yanga 3-0 Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment