March 23, 2018


Kocha wa Timu ya Taifa, 'Taifa Stars' Salum Mayanga, amekanusha uvumi wa taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa hajahusika na uteuzi wa kikosi cha Taifa Stars.

Taarifa hizo zimeibuka leo asubuhi ikiwa ni siku moja baada ya kikosi hicho kupoteza mchezo wa kirafiki usiku wa jana kwa mabao 4-1 dhidi ya Algeria.

Mayanga amesema taarifa hiyo si sahihi na ina nia ya kuvuruga kikosi, huku akieleza kuwa yeye alihusika kuteua kikosi na Kocha Msaidizi, Hemed Morocco alihusika kukitangaza.

"Taarifa inayozunguka mitandaoni kuwa sichagua timu ya Taifa siyo sahihi, ni upotoshaji wenye nia ya kutuvuruga. Watu waache kuupotosha umma, mimi ndiyo nimechagua kikosi chote kilichosafiri kwenda Algeria na si mwingine. Kocha Hemed Morocco nilimuachia jukumu la kukitangaza baada ya uteuzi" amesema Mayanga.

Asubuhi ya leo zilisambaa taarifa hizo zikieleza Mayanga hajahusika na uteuzi wa kikosi cha Stars huku zikidai Kocha Msaidizi, Hemed Morocco ndiyo alihusika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic