Mfaransa wa Simba, Pierre LEchantre ambaye ndiye bosi wa benchi la ufundi, amemuonya kiungo wake, Mohammed Ibrahim kwamba lazima ajue Simba si sehemu ya kujifurahisha.
Lechantre amemtaka kiungo huyo kuhakikisha anafanya kazi kwa juhudi na si kuifanya Simba kama sehemu ya mapumziko au kujifurahisha.
“Hapa si sehemu ya holiday, lazima ajue kuwa sisi tuko makini na lazima awe makini. Anachotaka kufanya hakitakubalika hata kidogo.
“Nashangazwa sana na anachotaka kukifanya, leo ana hiki, kesho ana lile. Sitaki hilo,” alisema.
Lechantre amesema Mo Ibrahim amekuwa mtu asiye makini na kama ataendelea na tabia hiyo atashindwa kufanya naye kazi.
Suala hapa ni kuwepo mazoezini. Kocha hakubali kutohudhuria mazoezi kwa visingizio kibao, mara nauguliwa na mke wangu, mara mtoto sasa haya yanarudisha nyuma maendeleo ya timu lakini kusema kweli hata mchezaji mwenyewe unakosa mazoezi unarudi nyuma ndio maana mwalimu anasema mara mbili mara tatu siwezi kukubali. Yupo sawa. Mo Ibrahim zingatia maelekezo ya mwalimu hakika utafika mbali wewe una uwezo mkubwa na kipaji cha kuucheza mpira.
ReplyDeleteInawezekana Mo ana matatizo binafsi yanamchanganya ila mpira ndio kazi yake na wazungu wapo profession zaidi katika kazi huwa hawana kumumunya kukwaambia ukweli na ndio maana hata wachezaji wetu wanapokwenda nje kujaribu kucheza kule huishia kushindwa na kurudi nyumbani si kwamba hawana uwezo kimpira la hasha, nidhamu kwa wachezaji wetu ndio tatizo kubwa yaani kujituma kuliko tukuka hasa mazoezini na kufuata maelekezo ya waliimu kikamimifu . Wazungu wanaamini unapokuwa na matatizo yako binafsi unatakiwa kuyaacha nyumbani kwa asilimia mia moja100% na kuendelea kuchapa kazi kana kwamba huna matatizo yeyote yale. Lakini inawezekana kwa mtanzania ukimwambia aache matatizo yake nyumbani na ajali kazi zaidi anaweza kuona unamnyanyasa na si ajabu akachukua maamuzi ya kuachana hata na hiyo kazi . Kazi ya mchezo wa mpira ni kazi ngumu sana. Ugumu wake unakuja pale utendaji wake unapofanyika hadharani mubashara kila mtu anaona unafanya nini na kwa kiwango gani? Kwa maana hiyo hakuna mtu mwenye wakati mgumu zaidi katika maisha ya kazi ya mpira kama kocha. Mara nyingi kufeli kwa timu au hata mchezaji lawama zinakuja kumuangukia kocha hata kama uzembe ulikuwa wa wachezaji au mchezaji . Kwa kocha wa Simba kufuatilia tabia za mchezaji mmoja mmoja binafsi tena kwa kipindi kifupi inaonesha jinsi gani alivyo serious na kazi yake lakini kubwa zaidi inaonesha ni kocha mwenye hamu ya kutaka kuona vijana wake wote wanafanikiwa na kuwa msaada kwa timu na maisha yao binafsi kwani kiuhalisia pengo la kukosekana huduma ya Mo katika kikosi cha Simba halipo hivi sasa . Pale Simba pana ushindani wa namba kweli kweli ila bila ya kumumunya maneno kwa wale wachezaji wasiobahatika kupata namba hawatakiwi kusubiri bahati wanatakiwa kupambana kiume bila ya aibu kupandisha viwango vyao hatimae kuwapa pressure wachezaji wanaohisi wana namba za kudumu. Mlipili ni moja kati ya wachezaji wa kupigiwa mfano kuonesha yakwamba hakuna kisicho wezekana.
ReplyDeleteNa majuzi amesaini mkataba mpya kwa dau alilokubali mwenyewe....MO itendee haki huo mkataba uliosaini
ReplyDeleteNI wakakati wa Mohamed Ibrahim (MO) kujirekebishsa kwani pamoja na SIMBA kuwa na kikosi kipana ana uwezo wa kupata NAMBA ya kudumu na kuisaidia time . Mimi binafsi namkubali kwa kiwango alichokuwanacho kabla na kwa umri wake , azingatie ushauri wa kocha atafanikiwa.
ReplyDeleteArudishe pesa za usajili, afukuzwe na angoje kusajiliwa na yanga ambao wanamraka ili akastarehe kwa marupurupu pamoja na Hajib na Hasan Kesi
ReplyDelete