March 1, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumatano ya jana, kikosi cha Yanga kimerejea salama jijini Dar es Salaam.

Yanga walikuwa mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo huo wa ligi ambao umewapa matokeo chanya na kuwasaidia kufikisha alama 40 na kufanya tofauti yao na Simba anayeongoza ligi kuwa pointi 5.

Baada ya kutua Dar es Salaam, kikosi cha Yanga kitaanza maandalizi ya hatua inayofuata ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Ikumbukwe Yanga walisonga mbele kwenye mashindano haya baada ya kuiondosha St. Lous FC ya Ushelisheli kwa jumla ya mabao 2-1.

Yanga itacheza na Township Rollers Machi 6, 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic