Mechi ya Ligi Kuu nchini Ugiriki imesitishwa ghafla baada ya mmiliki wa timu moja iliyokuwa inacheza kuingia na bastola uwanjani akitaka kumfyatulia mwamuzi.
Mechi hiyo kati ya Paok Salonika dhidi ya AEK Athens ilivunjika dakika za nyongeza baada ya Paok kupata bao dakika za nyongeza lililofungwa na Ferndando Varela.
Wakati huo Paok walikuwa nyuma kwa bao 1-0 na hilo lilikuwa bao la kusawazisha. Lakini mwamuzi alisema halikuwa sahihi sababu ilikuwa ni offside.
Mmiliki wa Paok, Ivan Savvidis ambaye ni mfanyabiashara mkubwa nchini Ugiriki aliamua kuingia uwanjani akiwa na bastola yake tayari kufyatua.
Hata hivyo zilifanyika juhudi kubwa kumuwahi na kumzuia aisitimize alichotaka kukifanya. Walinzi wake ndiyo waliofanya kazi hiyo kuhakikisha wanamdhibiti.
Mashabiki walitakiwa kutoka na kwenda makwao mara tu baada ya mechi hiyo kutoendelea.
Hata hivyo kulikuwa na mkanganyiko kwamba mwamuzi Giorgos Kominis alilikubali bao hilo lakini kukawa na hali ya kutoeleweka.
AEK walikuwa kileleni kwa tofauti ya pointi 3 dhidi ya Paok jambo lilimfanya mmiliki huyo kuona kama wanaonewa.








0 COMMENTS:
Post a Comment