March 2, 2018


Wakala wa mchezaji Muitaly, Mario Balotelli, Mino Raiola, amesema kuwa mchezaji wake anaweza akarejea katika Ligi za Italy na Uingereza endapo watakubaliana.

Raiola ametaja kiasi cha  paund £88m ndicho kitakachomtoa Nice ya Ufaransa na kumrejesha Uingereza ama Italy. 

Balotelli aliwahi kuvitumikia vilabu ya Manchester City na Liverpool vinavyoshiriki ligi ya Uingereza na vilevile aliwahi kuchezea AC Milan na Inter Milan nchini Italy.

Balotelli alikuza zaidi jina lake wakati anaichezea Manchester City na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi katika msimu wa 2013 ikiwa chini ya Kocha, Roberto Mancini.

Wakala Raiola amesema tayari ameshazungumza na Juventus, Roma, Inter Milan na vilabu vingine Ulaya huku akisema Balotelli ni moja ya washambuliaji 10 bora duniani kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic