YANGA KUKIPIGA NA SINGIDA UNITED KOMBE LA SHIRIKISHO, DROO KAMILI IKO HIVI
Na George Mganga
Droo ya upangaji wa timu zitakazokuwa zinacheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho imefanyika asubuhi ya leo katika makao makuu ya Azam Tv yaliyopo Tabata, Dar es Salaam.
Upangaji huo ulihusisha timu nane ambazo ziliingia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, timu hizo ni Yanga, Stand United, Azam FC, JKT Tanzania, Mtibwa Sugar, Singida United, Njombe Mji na Tanzania Prisons.
Baada ya droo kupangwa, timu zitakozokutana katika hatua hii ni hizi
Singida United v Yanga
Tanzania Prisons v JKT Tanzania
Azam FC v Mtibwa Sugar
Stand United v Njombe Mji
Safari hii fa itawashangaza wengi.
ReplyDeleteEndeleni kupanga...kazi yetu ni mpira tu
ReplyDeleteEndeleni kupanga...kazi yetu ni mpira tu
ReplyDelete