TFF YATUMA MAOMBI TLS IKIOMBA WAKILI WA WAMBURA APIGWE 'STOP' MARA MOJA
Shirikisho la Soka nchini (TFF), limekiomba Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), kumzuia Wakili Emmanuel Muga, kumuwakilisha aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Richard Wambura, katika rufaa yake inayotegemewa kusikilizwa muda wowote kuanzia wiki hii.
Taarifa hiyo iliyosambaa inaeleza kuwa Wakili Emmanuel Muga alikuwa ana mkataba na TFF, na suala la Ndug. Wambura lilitendeka enzi za uhai wa mkataba wake.
TFF inaiomba TLS imuagize Muga asitishe mara moja uwakilishi wake katika mashauri mengine yanayoihusisha TFF na viongozi wake, wanachama au walalamikaji wengine ili kuondoa mgonagano huu wa kimaslahi.
Wakili Muga anamuwakilisha Wambura aliyefungiwa kujihusisha na masuala ya soka baada ya TFF kugundua kuwa aliutumia kinyume na matwaka fedha za shirikisho hilo, pamoja na makosa mengine mbalimbali.
0 COMMENTS:
Post a Comment