USTADH SALAH MAMBO YAKE YAZIDI KUWA SAFI, ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA EPL
Na George Mganga
Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Uingereza kwa mwezi Februari 2018.
Salah amehusika amehusika katika mabao 6 ambayo Liverpool ilifunga mwezi Februari, ambapo ametengeneza mawili na kufunga manne.
Hii ni tuzo ya pili sasa Salah anaitwaa akiwa na Liverpool msimu huu.
Baada ya kutwaa tuzo hiyo, Salah amesema amefurahi kupata zawadi hiyo na atazidi kuipigania Liverpool ipate pointi tatu pamoja na kuiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi.
"Ni furaha kushinda tuzo hii tena, nitazidi kuipigania timu yangu iweze kupata matokeo kwenye kila mchezo ili iwe wenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi" amesema Salah.
Wachezaji wengine waliokuwa wanawania tuzo hiyo ni Sergio Aguero, Mousa Dembele, Pascal Gross, Eden Hazard, Glenn Murray na Xherdan Shaqiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment