March 9, 2018


Na George Mganga

Chris Hughton ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu Uingereza kwa mwezi Februari 2018.

Kocha huyo anayeifundisha klabu ya Brighton & Hove Albion, ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.

Hughton amefanikiwa kushinda dhidi ya West Ham United na Swansea City katika Uwanja wake wa nyumbani mwezi Februari mwaka huu, huku akienda sare dhidi ya Stoke City.

Tuzo hiyo ameipata akiwa na miaka 59 sasa, ameshahusika katika michezo 121 ya ligi, akiwa amewahi kuzifundisha Newcastle United na Norwich City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic