March 31, 2018



Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, amesema maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Singida United yameenda vizuri leo.

Yanga ipo mjini Singida kwa ajili ya kibarua hicho dhidi ya Singida United katika Kombe la Shirikisho utakaopigwa Namfua Stadium.

Ten amesema wachezaji wote wako fiti ikiwemo Donald Ngoma, huku akieleza kuwa Kocha ndiye atakuwa ana majukumu ya kuamua kama amuanzishe au kutomuanzisha.

Aidha, Teni amesema wachezaji wote wako kwenye morali na ari kubwa na wako tayari kwa ajili ya pambano hilo litakalopigwa kesho majira ya saa 10 kamili jioni.

Mshindi wa kesho ataungana na Stand United, JKT Tanzania pamoja na Azam FC au Mtibwa Sugar katika hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic