April 20, 2018



Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameitaka klabu yake kufanya usajili ili kukiboresha kikosi hicho ambacho kina wachezaji kadhaa walio majeruhi.

Mzee Akilimali ameomba Yanga ifanye usajili huo katika nafasi tatu ili kuweza kukipa makali kiweze kurejea kama ilivyokuwa miaka miwili nyuma.

Mjumbe huyo amewataka Yanga kusajili beki mmoja ili asaidiane na Abdallah Shaibu 'Ninja', pia akiomba asajiliwe mchezaji namba 8 na 9.

Akilimali amefikia kutoa ushauri huo kutokana na namna mwenendo wa kikosi ulivyo hivi sasa ambapo imekuwa na wachezaji ambao ni majeruhi kama Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao hawajacheza kwa muda mrefu.

1 COMMENTS:

  1. Uyumzee inaonekana hayupo pamoja natimu mbonajambo hilo lilisha zungumzwa na mkwasa kwasasa timu ikuwa ikitumia vijana wake wa kikosi chapili na wachezaji wandani wanao maliza mikataba kwenye timu zao na sio wachezaji wa kigeni wenyegharama kubwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic