April 28, 2018




Na George Mganga

Kikosi cha Majimaji kimepanda nafasi moja juu kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Mao ya Majimaji yote matatu yamefungwa na Marcelo Bonventure katika dakika za 18,73 na 82 huku Ruvu wakijipatia la kufutia machozi kupitia kwa Fully Maganga katika dakika ya 60.

Ushindi huo unaifanya Majimaji ipande juu mpaka nafasi ya 14 kwa kufikisha alama 23.

Matokeo mengine ni Azam FC imetamba ugenini mbele ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Turiani kwa kuibuka na bao 1-0. Bao pekee limetiwa kimiani na Shaban Idd kwenye dakika ya 43.

Mechi nyingine ilikuwa kati ya Stand United waliokuwa wakiikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga uliomalizika kwa sare ya 0-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic