YANGA YATOA ONYO HILI KWA WAAMUZI WA KESHO
Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka Waamuzi watakaochezesha mchezo wa kesho dhidi ya Simba kufuata sheria 17 za mchezo wa soka.
Kauli hiyo imetolewa na Yanga kupitia Afisa Habari wa timu hiyo, Dismas Teni, ambapo kikosi chao kitakuwa mgeni dhidi ya Simba.
Teni ameeleza kuwa timu zimewekeza kwenye mpira hivyo haitopendeza kuona Waamuzi wanaharibu ladha ya mpira na ksuhindwa kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka.
Timu hizo zinakutana kesho ikiwa ni katika mzunguko wa pili wa ligi, baada ya ule wa kwanza kwenda sare ya bao 1-1.
Mechi ya kwanza mlibebwa simba walinyimwa penalty mbili za wazi kabisa
ReplyDeleteKabisa katika mechi za watani wa jadi za hivi karibuni Yanga wanekuwa wanufaika wakubwa na maamuzi ya marefafree sio zamabi kambi tutasema yanga huwa inabebwa. Unakumbuka Amis tambwe alivyoudaka mpira na kuuweka mguuni na kufunga bao. Au unaikumbuka kadi nyekundu Jonas Mkude ambayo TTF wakaifuta lakini tayari uharibifu ulishafanyika kwa upande wa Simba. Au unakumbuka Ngoma alivyompiga kiwiko Ramadhani kessy wakati huo bado anachezea simba lakini hakuna chochote kilichotokea kwa Ngoma? Basi hiyo ni mifano michache tu jinsi gani yanga ilifaidika na maamuzi ya utata ya maarefa katika mechi zake na Simba za hivi karibuni.
ReplyDeleteTunahitaji moyo wa aina hiyo. Siku zote martefa wamelalamikiwa na vilabu vyetu vikubwa. Jibadilini marefa acheni kuumiza timu msizozishabikia muwe FAIR tu.
ReplyDelete