April 26, 2018



Wakati kikosi cha Yanga kikiendelea na mazoezi mjini Morogoro kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, uongozi wa timu hiyo umewapiga somo la kisaikolojia wachezaji wake kabla haijavaana na Simba.

Taarifa zinaeleza kuwa benchi la ufundi la Yanga limekaa na wachezaji kuwapa somo kuelekea mechi ligi dhidi ya watani Simba itakauopigwa Aprili 29 2018.

Benchi hili kupitia Kocha Msaidizi Shadrack Sanjigwa limewaambia wachezaji wanapaswa kuwa watulivu na kuuchukulia mchezo huo kama michezo mingine ya ligi.

Benhi hilo la ufundi limewatia hamasa wachezaji haswa katika namna ya kupambana uwanjani ili kikosi kiweze kupata matokeo dhidi ya Simba.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya mechi tayari kukipiga na vinara wa ligi Simba Jumapili ya wiki hii.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic