NIYONZIMA AWATAKA WANASIMBA WASIWE NA WASIWASI KUHUSU YANGA, AMEFUNGUKA HIVI
Kiungo wa klabu ya Simba aliyeondoka jana kuelekea kwao Kigali, Rwanda, Haruna Niyonzima, amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kuelekea mechi dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga.
Kauli hiyo ameitoa Niyonzima ikiwa ni saa chache zimesalia kuelekea Kigali kuhudhuria msiba wa dada yake, Sumaya Twizemana aliyefariki jana baada ya kuumwa.
Akizungumza na kipindi cha Spoti Leo kupitia Radio One, Niyonzima alieleza kuwa mashabiki wa Simba hawapaswi kuwa na wasiwasi kutokana na kikosi chao kuwa kipana hivyo watapambana kupata matokeo.
Kiungo huyo anaamini kuwa ushindi huo utakuwa chachu ya kuchukua ubingwa msimu huu kutokana na timu yake kuukosa kwa muda mrefu.
Aidha, Niyonzima alisema kuwa anatambua wapenzi wa Simba walitamani kumuona Uwanjani lakini haitowezekana kutokana na tatizo lililomsibu.
Simba itakuwa mwenyeji wa pambano hilo litakalofanyika Jumapili ya Aprili 29 2018 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment