April 19, 2018



Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir haroub 'Cannavaro', amesema kuwa kitita cha pesa ambacho ni kiasi cha zaidi ya milioni 600 watakazopewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zitasaidia kunusuru changamoto za klabu.

Cannavaro ameeleza kuwa ni kweli Yanga hivi sasa wanapitia wakati mgumu ukiachana na miaka kadhaa iliyopita, haswa katika suala la kuyumba kwa uchumi ndani ya klabu.

Mchezaji huyo anaamini milioni 600 zitasaidia kutatua matatizo mbalimbali ambayo wanakumbana nayo hivi sasa ili kusaidia kurejesha morali nzuri kikosini.

Yanga itapokea fedha hizo kutokana na kuifungashia virago Wolaita Dicha SC na kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa jumla ya mabao 2-1.

CHANZO: EFM RADIO

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic