April 19, 2018



Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, amewapongeza wachezaji wenzake kwa kuiwezesha timu kufuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuiondoa Wolaita Dicha SC kwa idadi ya mabao 2-1.

Licha ya kufungwa kwenye mchezo wa jana kwa bao 1-0, Tambwe amefurahishwa na ushindi huo ambao ni muhimu zaidi kwa Yanga.

Mbali na furahi hiyo, Tambwe ameeleza pia kuwa anaumia sana kuendelea kuuguza majeraha sababu inayopelekea ashindwe kucheza mpaka sasa.

Vilevile amewashukuru wanachama na wapenzi wa Yanga kwa kuzidi kumtia moyo haswa kipindi hiki akiwa hajakaaa sawa kiafya.

"Nawapongeza wachezaji wenzagu kwa kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi, Nawashukuru wanayanga kwa jinsi wanavyonisapoti wakati huu wa majeraha yangu,naumia sana kutokucheza lakini hili ndiyo soka" amesema Tambwe. 

1 COMMENTS:

  1. Waambie mabosi wako wakupeleke India wasikutake wakati ukiwa mzima tu bali hata unapokuwa mgonjwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic