April 22, 2018



Wakati kikosi cha Yanga kikiwa tayari kukabiliana na Mbeya City leo, wachezaji waliokuwa majeruhi ikiwemo Ibrahim Ajibu na Andrew Vincent wako fiti kucheza leo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Teni, amesema kuwa wachezaji wote wamepona hivyo ni jukumu la Kocha kuamua nani acheze na yupi asicheze.

Vincent na Ajibu walishindwa kuungana na Yanga katika safari ya kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha SC kutokana na kuwa majeruhi.

Lakini kwa taarifa zilizotoka ndani ya uongozi kuna uwezekano mkubwa wakawa sehemu ya mchezo dhidi ya Mbeya City leo.

Yanga itakuwa inacheza na Mbeya City kuendeleza harakati zake za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu ikiwa na alama 47 dhidi ya vinara Simba walio na 59.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic