April 22, 2018



Kuafuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC waiyoipata Simba jana katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom, Nahodha wa timu ya Simba, John Bocco, akiri mechi ilikuwa ngumu.

Bocco ameshukuru walau wamepata alama moja ambayo inashindwa kuwaharibia rekodi yao ya kutokupoteza mchezo mmoja mpaka sasa katika ligi.

Akizungumza baada ya mechi kumalizika, Bocco alieleza kuwa mechi ilikuwa ngumu huku akisema wapinzani wao walikuwa vizuri.

Mbali na hayo, Bocco alieleza kuwa hivi sasa watajipanga zaidi na mchezo unaofuatia dhidi ya Yanga ili kuweza kulipambani taji ambalo wamelikosa kwa takribani zaidi ya misimu minne.

Baada ya mchezo huo, Simba itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam dhidi ya watani wao wa jadi Yanga katika mechi inayofuata itakayopigwa Aprili 29 2018.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic