April 22, 2018





Ikiwa ni siku kadhaa zimesalia kuelekea pambano la mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Lipuli FC dhidi ya Simba SC lililopigwa jana katika Uwanja wa Samora, mjini Iringa, kulizuka maneno kuwa timu hiyo itaifanyia ushikaji Simba ili ipate matokeo.


Kocha Msaidizi wa Lipuli, Seleman Matola, amezungumzia uvumi huo ambao ulisambaa kwa kusema hayo ni maneno tu ya mtaani.

Matola alieleza kuwa watu walianza kuzungumza maneno kama hayo kutokana na kwamba aliwahi kuifundisha Simba akiwa Kocha Msaidizi kwa muda mrefu.

"Unajua kuna watu wanapenda kuzusha maneno ambayo si ya kweli, mpira ni sehemu ya kazi, na hayo yamekuja kutokana na kuwa niliwahi kuitumikia Simba kama mchezaji na Kocha" alisema.

Mechi iliyopigwa jana ilimalizika kwa sare ya 1-1 huku Lipuli wakifunga kupitia Adam Salama na Simba kupitia Laudit Mavugo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic