Msemaji wa Klabu ya simba Haji Mnara na Mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Diffa El Jadida ya nchini Morocco Simon Msuva wametoa pole kwa Watanzania ambao wamegusa na msiba huo.
Agness Masogange ambae alikuwa ni video queen aliyetikisa kwenye nyimbo mbalimbali hasa ya Belle 9 amefariki dunia jana katika hospitali ya Mama Ngoma baada ya kuumwa ghafla na kukimbiza katika hospitali hiyo.
Mwili wa Masogange umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili huku taratibu za mazishi zikendelea ambapo mwili wake wanatarajiwa kumpumzishwa kwao Mbeya.
CHANZO: GLOBAL TV
0 COMMENTS:
Post a Comment