April 4, 2018




Kiungo mkabaji wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo wiki iliyopita ilikuwa mbaya kwake baada ya kukosa moja ya penalti za kikosi chake walipokuwa wanacheza na Singida United ambapo baada ya mchezo huo ambao Yanga walitolewa, kiungo huyo hakuweza kula chakula cha usiku kutokana na kuumizwa na kitendo hicho.

Tshishimbi alikosa penalti hiyo ya kwanza ya Yanga katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), walipokuwa wanacheza na Singida United wanaofundishwa na Kocha Hans van Der Pluijm, uliopigwa Uwanja wa Namfua, Singida huku Yanga wakipoteza kwa penalti 2-4. Penalti nyingine ya Yanga ilikoswa na kiungo Emmanuel Martin.

Chanzo kutoka ndani ya kikosi hicho kimesema, kuwa Mcongo huyo alifikia hatua hiyo ya kutokula usiku kutokana na kuumizwa na kitendo hicho cha kuisababisha timu yake isukumwe nje ya kombe hilo.

"Baada ya mechi ile na Singida United wachezaji wote walikuwa na hali mbaya kutokana na kile ambacho kimetokea lakini ambaye alikuwa zaidi ya wenzake ni Papy Tshishimbi ambaye yeye kwa usiku huo hata kula kumlishinda kwa sababu ya kukosa ule mkwaju wake wa penalti.


"Lakini uongozi ulijitahidi kuwaweka sawa na kuwarudisha katika hali ya kupambana kwenye mechi zijazo na kusahau mechi hiyo na kila kitu kinaenda sawa kwa sasa mawazo yote yapo juu ya mchezo wetu unaokuja dhidi ya Wolatya Dicha," kilisema chanzo hicho.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic